HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 5 Juni 2018

Usajiri yanga

Wakati baadhi ya timu zikiwa 'busy' kufanya usajili sasa ambapo hata dirisha la usajili bado halijafunguliwa, hali ni tofauti kwa Yanga.

Klabu ya Yanga imeficha mchakato wake wa usajili tangu ilipobainisha kutaka kumchukua aliyekuwa mshambuliaji wa Lipuli Fc Adam Salamba ambaye hata hivyo zilifanyika 'figisu' kutoka kwa viongozi wa Lipuli FC kuhakikisha mchezaji huyo anatua Simba.

Msimu uliopita Yanga ilikumbwa na 'presha' ya usajili iliyozikumba timu nyingine msimu huu na kujikuta inasajili bila mpangilio.

Katika msimu huo, mbali ya kusajili wachezaji wengi chipukizi, Yanga iliongeza mikataba ya Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko ambao hata hivyo hawakuweza kuisaidia timu hiyo kutetea ubingwa wake kwa msimu wa nne mfululizo.

Wakati Kamusoko akirejea kikosini msimu ukielekea ukingoni, Donald Ngoma na Amissi Tambwe ni kama walikula mishahara ya bure msimu mzima kutokana na majeruhi.

Yanga ilizinduka wakati kumekucha na kuvunja mkataba wa Ngoma ambaye tayari ametua klabu ya Azam FC. Hawa Azam nao watakuwa wamekumbwa na presha ya usajili!

Usajili wa 'pupa' uliofanywa na Yanga msimu uliopita ulipelekea mabingwa hao wa Kihistoria wa Tanzania kushindwa kutetea ubingwa wao kwa msimu wa nne.

Mwaka huu hali ni tofauti, Yanga imeongeza umakini kwenye zoezi la usajili japo hali hiyo inawatia hofu mashabiki wake wengi waliokuwa wamezoea usajili wa mbwembwe.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amenukuliwa na mtandao wa Mwanaspotiakisema kuwa hawana presha ya kusajili kwa sasa wanasajili taratibu na kwa umakini zaidi ili kukwepa changamoto ya kujaza majeruhi katika kikosi chao kipya.

Saleh amesema usajili wa Yanga msimu huu unalenga zaidi kuziba nafasi zilizokuwa na matatizo msimu uliopita huku akiweka wazi kuwa hawasajili kutokana na upepo wa wachezaji waliofanya vizuri msimu huu bali wanafuata ripoti ya mwalimu inasemaje.

"Unajua kumekuwa na maneno mengi kuwa Yanga msimu huu haina fedha na ndio maana haifanyi usajili siyo kweli tunaangalia kwa umakini na tupo katika mikakati imara zaidi kuhakikisha tunafanya usajili bora zaidi kulingana na mahitaji." 

"Msimu uliopita tulikuwa tunakabiliwa na majeruhi wengi ndio walikuwa wachezaji tegemezi katika kikosi jambo ambalo lilisababisha kushindwa kuionyesha ushindani hivyo kwasasa tunaangalia mambo mengi kabla ya kumsajili mchezaji kwa lengo la kukwepa changamoto hiyo."

Yanga huenda ikaibuka na kikosi bora zaidi kwa kuwa wamejipa muda wa kufanya usajili utakaokidhi mahitaji tofauti na baadhi ya timu ambazo zinasajili wachezaji ili kuwafurahisha mashabiki wao.