Baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Ruvu Shooting kwenye mchezo wa kwanza wa michuano ya Uhai Cup, kikosi cha pili cha Yanga leo kinashuka dimbani mkoani Dodoma kucheza na Mbao FC.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa nane mchana katika viwanja vya chuo kikuu cha Dodoma.
Yanga iko kundi A pamoja na timu za Ruvu Shooting, Mbao FC na Mbeya City.
Mbao FC inaongoza kundi hilo ikiwa na alama 3 ikifuatiwa na Yanga, Ruvu Shooting zote zikiwa na alama moja moja.
Mbeya City inaburuza mkia.