BREAKING: Elizabeth Michael ‘Lulu’ ahukumiwa kifungo jela
Mahakama Kuu Dar es Salaam, imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela, muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael, maarufu ‘Lulu’, baada ya kumkuta na hatia ya kuua bila kukusudia. Hukumu ya kesi hiyo imesomwa mapema leo na Jaji wa Mahakama Kuu, Sam Rumanyika, ambaye baada ya kusikiliza utetezi kutoka kwa mawakili wa upande wa mshtakiwa aliitoa hukumu hiyo.
Lulu, alishtakiwa kwa kesi ya kumuua bila kukusudia, aliyekuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini na nje ya nchi, Steven Kanumba ambaye alikuwa mpenzi wake.
Wakili Peter Kibatala, aliyekuwa anamtetea Lulu amesema kuwa watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake.