HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 14 Novemba 2017

Mhasibu TAKUKURU Anayemiliki Mali Nyingi Katoroka....... Atakayempata Kuzadiwa Milioni 10


Mhasibu TAKUKURU Anayemiliki Mali Nyingi Katoroka..Atakayempata Kuzadiwa Milioni 10




                  Taasisi ya Kuzuia na  Kupambana na Rushwa (Takukuru) imetangaza donge nono la Sh10 milioni kwa yoyote atakayefanikisha kukamatwa kwa aliyekuwa mfanyakazi wake Godfrey Gugai.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Novemba 14, Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali, John Mbungo amesema Gugai anatuhumiwa kujipatia mali nyingi  kinyume cha Sheria ya  Utumishi wa Umma.

Amesema kwa nafasi ya Gugai ya  mhasibu wa taasisi hiyo ni vigumu kupata mali nyingi kiasi hicho.

"Awali tulipomhoji alitoa ushirikiano lakini tukiwa tunaendelea alitoweka na kwa taarifa tu amekuwa akitoka kwa magendo nje ya nchi, kwa yeyote atakayefanikisha kumpata tutamzawadia Sh10 milioni," amesema  Mbungo

Amesema baada ya kutoweka walikwenda mahakamani kuhusu mali zake na tayari kuna zuio la kutokufanya kitu chochote yaani visiuzwe au kuendelezwa.

Baadhi ya mali anazomiliki mtuhumiwa ni pamoja na nyumba ya ghorofa nne iliyopo Ununio; nyumba ya ghorofa tatu iliyopo Bunju; nyumba za kupangisha zilizopo Mbweni JKT zote zikiwa jijini Dar es Salaam.

Nyumba nyingine iko Majita, Musoma;  nyumba mbili zikiwa Kiseke na Nyegezi, Mwanza.

Zaidi ya nyumba hizo, anamiliki viwanja maeneo ya Bunju, Kigamboni, Mbuyuni-Temeke mkoani Dar es Salaam;  Bagamoyo, Kibaha mkoani Pwani;  huko Morogoro ana kiwanja huko Kihonda, Kiegea na Lukobe.

Viwanja vingine viko Kisasa, Itege na Kidachi mkoani  Dodoma;  vingine viko Nyegezi, Nyamanoro na Nyamagana mkoani Mwanza; ambapo ana viwanja vingine mikoa ya Musoma, Arusha, Tanga na kwengine.

"Kama atakuja na kutupa ushirikiano ikiwamo kuthibitisha uhalali wake basi tutamwachia mali yake lakini kwa nafasi yake kumiliki mali zote hizi zinatutia walakini," amesema

Naibu mkurugenzi huyo amewaonya watumishi wa umma kutokutumia vibaya madaraka yao waliyopewa kwani wakibainika hawatasita kuwachukulia hatua.