HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 21 Novemba 2017

MWENYEKITI WA BAVICHA AHAMIA CCM



Mwenyekiti wa BAVICHA Aibwaga Chadema Ahamia CCM


Mwenyekiti wa Bara la Vijana Chadema Taifa , (BAVICHA) Patrobas Katambi ameomba ridhaa ya kujiunga na ChamaCha Mapinduzi CCM, leo kwenye kikao cha Halmashauri Kuu Taifa NEC kwa madai kwamba siyo kwa sababu ya madaraka bali kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Akizungumza mbele ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Ndg John Pombe Magufuli, Katambi amesema kwamba yupo tayari kuitwa msaliti kwa kusaliiti ubinafsi na kundi la mabinafsi kwa ajili ya maslahi ya taifa.


Akizidi kuomba ridhaa ndani ya Chama hicho Katambi amesema kwamba siasa za upinzani zimegubikwa na ubinafsi, umimi pamoja na makundi ya hapa na pale.
"Naomba ridhaa ya kuwa mwanachama siyo kwa sababu ya madaraka bali kwa ajili ya maslahi ya taifa pamoja na kusaidiana na wenzangu kukiendeleza chama. Natambua harakati zilizofanyika kwenye awamu iliyopita.



Watu wengi wanapenda lakini Hatupendi kubadilika na Mabadiliko yabnapoanza misuguano ndipo inapoanzia....." Katambi Kwa upande mwingine Katambi amesema kwamba ameona CCM inawapatia vijana nafasi na fursa za kuongoza tofauti na alipotoka kwamba vijana wakishatumiwa wanaonekana kama takataka yaani karai baada ya ujenzi.