HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatano, 13 Desemba 2017

CHADEMA Ajitoa Rasmi Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Songea Mjini

CHADEMA Ajitoa Rasmi Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Songea Mjini

ZIKIWA zimepita siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Mheshimiwa Freeman Mbowe kutangaza kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani utaofanyika Januari 13, mwakani kwa majimbo matatu na kata sita chama hicho mkoa wa Ruvuma kimetangaza kuunga mkono tamko hilo na kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Songea mjini.

Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa Ruvuma Bw. Erenius Ngwatura amesema wanaunga mkono tamko lililotolewa na Mwenyekiti wao wa taifa wa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Mbowe na kubainisha kuwa uchaguzi wa udiwani uliopita kwa kata 43 uligubikwa na dosari kadhaa.

Kaimu Katibu wa CHADEMA jimbo la Songea mjini Bw.Masumbuko Mbogoro amesema sababu nyingine ya wao kujitoa kushiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Songea mjini ni kutokana na maombi yao kwa tume ya uchaguzi ya kutaka uchaguzi usogezwe mbele kutosikilizwa.

CHANZO: ITV