HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Ijumaa, 13 Aprili 2018

ALIYEZAA NA MCHINA, PAPARAZI WAACHA

ALIYEZAA NA MCHINA, PAPARAZI WAACHA 

Wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiendelea na zoezi la kuwasaidia wanawake waliotelekezewa watoto na wanaume pamoja na wanaume wenye matatizo na wake zao, pamoja na zoezi hilo kugubikwa na matukio mengi, gumzo zaidi limeachwa na mwanadada Safina Mohamed aliyezaa na raia wa nchini China pamoja na mpigapicha (paparazi) maarufu Ilala, Vedasto Mdesa.

Wawili hao walifika kwa nyakati tofauti katika ofisi ya Makonda, juzi Jumanne huku kila mmoja akieleza matatizo yake lakini watu waliokuwa wakifuatilia tukio hilo waliguswa zaidi na matukio ya aliyezaa na Mchina pamoja na paparazi. “Yaani kwa siku hizi mbili tangu Makonda afanye hii operesheni tumeshuhudia matukio mengi lakini hili la aliyezaa na Mchina na paparazi linafurahisha na kuhuzunisha,” alisema Abdu Jumio, mkazi wa Magomeni Dar.

Akizungumza na mwandishi wetu, Safina ambaye alifika kwenye ofisi hizo za Makonda, Ilala jijini Dar, kwa siku ya pili baada ya awali kushindwa kufikisha hoja zake, alisema walikutana na mwanaume huyo raia wa China, maeneo ya Gongo la Mboto akifanya kazi Kampuni ya Hygen ambako walikuwa wanajenga nyumba za wanajeshi miaka mitatu iliyopita na baadaye kibali cha mwanaume wake kiliisha, akatoweka.

Naye paparazi maarufu wa eneo la Buguruni jijini Dar, Vedasto Mdesa mkazi wa eneo hilo alisema amefika ofisini hapo ili kueleza jinsi alivyokimbiwa na mkewe. “Mimi na mke wangu tulibahatika kuzaa watoto watatu, tunapendana lakini familia yake ndiyo haikukubali mimi kumuoa mwanamke huyo, kwa sababu familia yangu kuwa ya kimaskini na mke wangu kutoka katika familia ya kitajiri, namuomba Makonda anisaidie niweze kurudishiwa familia yangu,” alisema paparazi huyo.

Jumatatu iliyopita, Makonda aliwaita wanawake wafike ofisini kwake kwa ajili ya kuwasaidia kisheria ambapo umati mkubwa wa wanawake ulijitokeza, Makonda akawataka wanaume waliotajwa na wanawake zao wafike ofisini kwake kwa ajili ya kusikiliza mashauri yao huku akiwataka wanaume ambao nao wana malalamiko kwa wanawake zao wajitokeze kulalamika.