Ukurasa wa Twitter wa As Roma umeandika hivi “tutakuwa wapinzani kwa dakika 180, lakini lolote litakalotokea tutaendelea kuwa marafiki milele” huo ni ujumbe kutoka kwq As Roma kwenda kwa Mo Salah.
Roma wameamua kumtumia Salah ujumbe huo baada ya ratiba ya nusu fainali ya Champions League kutoka na As Roma kujikuta mikononi mwa Liverpool ambayo ndio timu anayochezea Mo Salah kwa sasa.
Liverpool wana rekodi nzuri sana mbele ya As Roma, wamepoteza mechi moja tu kati ya tano dhidi yao, wakisuluhu mbili na kushinda mbili ikiwemo fainali ya European Cup 1983/1984 ambapo Liverpool walishinda kwa matuta.
Bayern Munich nao wameangukia tena kwa Real Madrid, hili ni bundi ambalo Bavarians hawataki kusikia. Katika michezo mitano ya mwisho ambayo Real Madrid wamekutana na Bayern Munich wameshinda yote.
Ukiacha rekodi ya Cristiano Ronaldo ya mabao 9 katika mechi 6 dhidi ya Bayern Munich lakini gwiji wa zamani wa Bayern Munich Roy Makaay anashikilia rekodi ya goli la haraka zaidi UCL(sekunde 10.12) ambalo alilifunga katika mechi hii.
Michezo hii ya nusu fainali ya Champions League itapigwa tarehe 24 mwezi April na baadae watarudiana tarehe 1 mwezi May kutafuta wababe wawili watakaoenda Kyiv kwa ajili ya fainali.