HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumapili, 29 Aprili 2018

Asante Kwasi Kuhusubiri kwa Hamu Mchezo wa Simba, Yanga



WAKATI Simba na Yanga zikitarajiwa kuvaana leo Jumapili ya Aprili 29, beki Mghana wa Simba, Asante Kwasi, amefunguka anajisikia furaha kucheza mchezo huo ambao ni mara yake ya kwanza na anaamini watapata matokeo.

Simba na Yanga zitashuka dimbani leo Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati mchezo wa awali uliozikutanisha timu hizo zilitoa sare ya 1-1.

Akizungumza na Championi Ijumaa, beki huyo alisema ni mchezo wake wa kwanza akiwa Simba lakini anajisikia furaha kuwa sehemu ya mchezo huo na lengo ni kupata matokeo.

“Najisikia furaha sababu ni mchezo mkubwa kwa timu zetu hapa nyumbani na kwa upande wangu, ni mara ya kwanza kucheza mchezo huo tangu nijiunge na Simba.

“Ingawa si mgeni kwa hizi timu sababu tayari awali niliwahi kukutana nazo nje ya hapa Simba, lakini kikubwa na sisi kupambana na kuweza kupata matokeo na kusonga mbele,” alisema Kwasi.