HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 30 Aprili 2018

Lissu kutua Dar es Salaam


MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa nchini Ubelgiji anatarajiwa kurudi nyumbani siku yoyote kuanzia juzi, baada ya madaktari kumaliza kumpatia matibabu, amesema.
tundu lissu.
Lissu ambaye amekuwa hospitalini tangu Septemba 7, mwaka jana aliposhambuliwa nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma, aliliambia shirika la utangazaji la BBC juzi, kuwa kwa sasa hana tena kidonda cha risasi na yupo tayari kurudi nyumbani.
"Sina tena kidonda cha risasi, nilipigwa mara 16," alidai Lissu (50) na kufafanua "sina tena kiungo kilichovunjwa".
"Nilikuwa nimevunjwa mguu mmoja mara tatu, mikono yote ilikuwa imevunjwa, nilikuwa na risasi nyingi mwilini, na vidonda vingi."
Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema viungo vyote vilivyokuwa vimevunjika vimeshaunga.
Alisema tangu aanze kupata matibabu amefanyiwa operesheni 17, nne zikiwa sehemu ya tumbo, lakini sasa hali yake ni nzuri.
Lissu alisema analazimika kurundi nchini kwa kuwa yeye ni Mbunge, Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri kivuli wa Sheria na Katiba.


BONYEZA HAPA CHINI ILI UWEZE

INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO

INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD KATISHA BLOG APP IN GOOGLE PLAY STORE ...ANDIKA KATISHA ...SEARCH


PATA HABARI KWA UHAKIKA ZAIDI NA KATISHA BLOG

Alisema kwa majukumu hayo hawezi kwenda mafichoni.
"Siwezi kwenda mafichoni, siwezi kuikimbia nchi yangu, nitarudi Tanzania," alisema.
"Mimi ni mbunge, mimi ni kiongozi bungeni, ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, mimi ni msemaji wa sheria na katiba wa chama changu."
Hata hivyo, akizungumza na Nipashe jana kaka wa Lissu, wakili Alute Mughwai alisema familia bado haijapokea taarifa ya siku anayotarajia kurudi.
Alisema familia inachofahamu ni kuwa Lissu amefanyiwa operesheni ya 19 wiki chache zilizopita, hivyo kutakuwa na uangalizi wa afya yake.
“Hayo mahojiano aliyofanya juzi sijayaona, nitawasiliana naye leo jioni (jana) nimsikilize, lakini sisi kama familia hatujapata taarifa yoyote lini atarudi, wala hatuwezi kujua hadi tupewe taarifa na hospitali,” alisema wakili Mughwai.
Lissu alipoulizwa na BBC endapo amepata msaada wa matibabu kutoka serikalini, alisema chombo pekee chenye wajibu wa kumgharamia matibabu yake ni Bunge na "siyo serikali, wala Ikulu, wala mtu yoyote."
Aprili 19 Spika Job Ndugai alilieleza Bunge kuwa matibabu ya Lissu yanagharamiwa na Serikali ya Ujerumani.
Ndugai alisema amefahamu hilo kwa kupewa taarifa na Balozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Waechter, lakini pia akataja masharti matatu yanayopaswa kuzingatiwa, ili Bunge ligharamie matibabu yake hayo ughaibuni.
Matibabu ya mbunge huyo yalianzia kwenye Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Nairobi, Kenya.
Chadema na familia yake wamekuwa wakilalama Bunge kukataa kugharamia matibabu ya mbunge huyo.
Hata hivyo, Spika Ndugai alieleza Bunge haliwezi kulipia gharama za matibabu za Lissu ughaibuni kwa kuwa hayakufuata taratibu za nchi ambazo wabunge na raia wa kawaida wanapaswa kuzifuata, ili serikali igharamiwe matibabu yao nje ya nchi.
Spika Ndugai alilazimika kutoa ufafanuzi huo bungeni kutokana na mwongozo ulioombwa kwake na Godbless Lema.
Mbunge wa Arusha Mjini Lema (Chadema), alitaka uongozi wa Bunge ueleze kwanini chombo hicho cha kutunga sheria hakitaki kugharamia matibabu ya Lissu.
Katika kujenga hoja yake, Lema alisema Lissu ana haki za kibunge na za raia wa kawaida kulipiwa gharama za matibabu na serikali, kama ilivyofanyika kwa Spika Ndugai ambaye ana siku chache tangu arejee nchini akitokea kwenye matibabu ya muda mrefu nchini India.
"Wakati Bunge la Bajeti likiendelea na vikao vyake, mbunge mwenzetu (Lissu) yupo Ubelgiji na Ofisi ya Spika bado inakataa kumlipia matibabu yake na haki zote za kimsingi anazo kama wewe (Spika),” Lema alisema na kueleza zaidi:
"(Spika) Ulipokuwa India kufanyiwa matibabu pamoja na ‘checkup’ (uchunguzi), serikali iligharamia matibabu yako. Mbunge bado yupo hospitali, lakini serikali haijaona wajibu.
“Kwanini serikali iligharamia matibabu ya Spika, lakini imeshindwa kuwajibika matibabu ya Lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi Septemba mwaka jana hapa Dodoma?”
Akimjibu mbunge huyo, Spika Ndugai alisema mara nyingi amekuwa akijizuia kuzungumzia jambo hilo kwa sababu Lissu yupo hospitalini, lakini ameona ni vyema alijibu, ili kuondoa mkanganyiko.
Alisema kuna namna mbili ambazo matibabu ya wabunge na wananchi wanaweza kutibiwa ughaibuni kwa kufuata utaratibu wa umma.
"Utaratibu ni kwamba anayekwenda kutibiwa nje hususani wabunge, ili ‘cheque’ (hundi) iandikwe, ni lazima kuwapo barua yenye kibali cha (Hospitali ya Taifa) Muhimbili, kwamba mgonjwa huyu anahitaji rufani na nchi ipi apelekwe,” Spika Ndugai alisema.
Alisema zaidi: "Pili, awe na kibali cha Wizara ya Afya na kwa wabunge kutibiwa nje lazima Spika nipate barua ya kibali kutoka kwa Rais.
“Nikishapata hivi vitatu ndipo Mhasibu wa Bunge anaweza kuandika hundi kwa mbunge yeyote kwenda kutibiwa nje ya nchi.”
Kiongozi huyo wa Bunge alisema wakati Rais John Magufuli akifungua Bunge la 11 Novemba 20, 2015, alieleza namna asivyoridhishwa na wabunge wanavyosafiri ovyo kwenda nje ya nchi.
SAFARI ZA OVYO
Alisema Rais alisema katika miaka mitano ya uongozi wake, moja ya mambo atakayosimamia ni kuzuia safari za ovyo nje ya nchi.
BONYEZA HAPA CHINI ILI UWEZE

INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO

INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD KATISHA BLOG APP IN GOOGLE PLAY STORE ...ANDIKA KATISHA ...SEARCH


PATA HABARI KWA UHAKIKA ZAIDI NA KATISHA BLOG
"Huo ndiyo utaratibu. Mhasibu wa Bunge au Katibu wa Bunge hawawezi kutoa fedha yoyote kama havijakidhi vitu hivyo vitatu. Mbunge yeyote anayetibiwa nje, ni wengi waliotibiwa, wote kwa awamu hii wamekwenda kwa utaratibu huo,” alisema.
"Kwa hili sasa Spika anaandikaje hundi?
“Wakati utaratibu wake (kumwondoa Lissu nchini), Lema hukuwapo, wenzako walikuwapo walipompeleka Nairobi walijua na walioamua ni pande mbili tu; alikuwa mwakilishi wa familia pamoja na viongozi wako wa Kambi (Freeman Mbowe na Mch. Peter Msigwa) ambao wote ni wajumbe wa Tume ya Huduma za Bunge ambayo inashughulikia matibabu ya wabunge.”
Spika Ndugai alisema uamuzi wa kumpeleka Lissu Nairobi ulikuwa ni uamuzi wa rufani binafsi ambao gharama zake hazipaswi kuwa za serikali.
Alisema kwa utaratibu wa matibabu binafsi, wapo wabunge wengi ambao wamekuwa wakienda nje ya nchi, akiwatolea mfano wabunge wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM); Charles Kitwanga (Misungwi) na Suleiman Nchambi (Kishapu).
"Kwa hiyo, ni kuchagua matibabu binafsi au ya umma. Ninyi (upinzani) mlichagua matibabu binafsi," Spika Ndugai alisema huku wabunge wa CCM wakimshangilia kwa kugonga meza.
Alisema hakuna mbunge yeyote anayebaguliwa na kama yupo, aeleze kama alifuata utaratibu huo na hakutibiwa kwa fedha za umma.
"Utaratibu ni utaratibu kwa watu wote. Kwa hiyo, tunashukuru hata hivyo, Wajerumani wanaomtibu Lissu kule Ubelgiji. Jambo hilo aliniambia Balozi wa Ujerumani,” alisema zaidi Spika Ndugai.
BONYEZA HAPA CHINI ILI UWEZE

INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO

INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD KATISHA BLOG APP IN GOOGLE PLAY STORE ...ANDIKA KATISHA ...SEARCH


PATA HABARI KWA UHAKIKA ZAIDI NA KATISHA BLOG