Azam FC imeendelea kusuasua katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kulazimishwa suluhu ya 0-0 na Njombe Mji katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Conplex, Chamazi.
Matokeo hayo yanaifanya iendelee kubaki nafasi ya tatu ikiwa na alama 46 ilizokusanya kutoka michezo 25.
Aidha matokeo ya michezo iliyopigwa mapema, Singida United ililazwa bao 1-0 na Lipuli FC huku Stand United ikiifumua Mwadui Fc kwa mabao 3-1.
Mbao FC na Majimaji zilitoshana nguvu kwa kutoka sare ya mabao 2-2.
Ligi hiyo itaendelea kesho Jumatatu kwa michezo mitatu kupigwa, Ndanda FC dhidi ya Ruvu Shooting, Kagera Sugar dhidi ya Mtibwa Sugar na Simba dhidi ya Prisons