HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 17 Aprili 2018

baada ya Diamond Platnumz kukamatwa na polisi na kuhojiwa kuhusu video chafu Nandi naye kukamatwa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema  kuwa tayari msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz jana Aprili 16, 2018 alikamatwa na polisi na kuhojiwa kuhusu video zake chafu alizosambaza kwenye mitandao ya kijamii.
Waziri Mwakyembe
Waziri Mwakyembe amesema hayo leo bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilombero, Goodluck Mlingwa aliyehoji jinsi gani serikali imejipanga kupambana na wasanii wa muziki pamoja na vikundi vya watu wanaosambaza lugha za matusi.

Waziri Mwakyembe amesema “Tulitunga sheria mwaka 2010 lakini tulikosa kanuni za kuweza kubana hasa maudhui upande wa mitandao, tumeshatunga hizo kanuni na sasa hivi hizo kanuni zimeanza kufanya kazi. Kuna baadhi ya wasanii wetu ambao walianza kufanya uhuni uhuni ndani ya mitandao ya kijamii jana tumeweza kumkamata msanii nyota Tanzania Diamond na tumemfikisha polisi na anahojiwa kutokana na picha chafu alizozirusha vile vile inabidi hata binti Nandy naye akamatwe ahojiwe,“amesema Waziri Mwakyembe.
Jana kwenye mitandao ya kijamii kulisambaa video ya msanii Diamond Platnumz akiwa faragha na wanawake wawili tofauti tofauti akiwemo mzazi mwenzake Hamissa Mobetto kitu ambacho kiliibua mijadala kibao wengi wakidai kuwa amewadhalilisha wanawake.

INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO


INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD KATISHA BLOG APP IN GOOGLE PLAY STORE ...ANDIKA KATISHA ...SEARCH