Ikiwa wewe ni mkazi wa Nairobi, epuka mitaa hii 12 kwa vyovyote vile
-Huenda ukaibiwa simu yake unapotembea katika baadhi ya mitaa Jijini Nairobi
-Inaaminika kuwa wezi na wahalifu hutembea katika maeneo kuliko na watu wengi
-Wengi hulenga watu ambao hawana ufahamu kinachoendelea na wanaotembea jijini au abiria ndani ya gari na kuiba simu
Kutembea katika mitaa ya Nairobi ukizungumza kwa simu huenda kukakutia hatarini. Hii ni kutokana na kuwa unaweza kupoteza simu hiyo kwa sababu ya wezi.

Ikiwa wewe ni mkazi wa Nairobi, epuka mitaa hii 12 kwa vyovyote vile. Picha/Mwakilishi
Wezi uhakikisha kuwa mawazo yako yako mbali kabla ya kutwaa simu na kutoroka hasa katika mitaa iliyo na shughuli nyingi.
Kulingana na Ma3Route, wezi hao huwa wanakaa katika vituo vya magari na mitaa mikubwa ambayo huwa na msongamano mkubwa wa magari.
Hii ni mitaa ambayo haufai kuchukua simu katu kama ilivyoorodheshwa na Ma3Route:
1. Sokoni Muthurwa na bus station
2. Tom Mboya street, kutoka Koja Mosque mpaka Afya Centre