HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumapili, 15 Aprili 2018

Israeli kuachia wafungwa 200 wahamiaji kutoka Afrika

Serikali ya Israeli imekuwa ikijaribu kufikia makubaliano na Uganda, ikiitaka nchi hiyo ya Afrika Mashariki iwapokee wahamaiaji hao, ambao waliingia nchini Israeli kwa kuvuka mpaka wa misri na nchi hiyo kwa miguu katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita

Shirika la habari la Reuters lilripoti Jumapili kwamba wengi wa wanaume hao mia mbili ambao wako karibu kuachiliwa, wamekuwa wakizuiliwa kwenye jela iliyo jangwani katika kipindi cha miezi michache iliyopita, wakisubiri kuhamishiwa nchini Uganda.

Siku ya Ijumaa, kwa mara ya kwanza, Uganda ilikiri kwamba inafanya mazungumzio na Israeli kuhusu suala hilo, lakini ikasema kuwa itawapokea tu wakimbizi ambao wataondoka Israeli kwa hiari yao na wala siyo kwa kuzlazimishwa.

Waziri wa majanga na maswala ya wakimbizi wa Uganda Musa Ecweru, alinukuliwa akisema kwamba Israel imeomba Uganda kuwapatia hifadhi wahamiaji wapatao mia tano walowasili kati ya mwaka 2006 na 2012.

Akizungumza na waandishi habari, waziri huyo alikanusha habari kwamba kuna mikataba ya siri  kati ya Uganda na Israel kuhusiana na suala hilo. Alisema maombi  ya watu hao 500 yanayojadiliwa hivi sasa yatakaguliwa kwa kina.

Ripoti ya shirika la kushughulikia wakimbizi la umoja wa mataifa UNHCR, ilisema  kwamba waafrika 4,000 waliokuwa wakitafuta hifadhi, wameondoka Israel kwa hiyari na kuelekea Uganda na Rwanda tangu mwaka 2013, ripoti ambayo Uganda na Rwanda zimekanusha.