Mchezo wa marudiano kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho kati ya Wolaitta Dicha dhidi ya Yanga utarushwa mubashara na runinga ya Azam kupitia chaneli ya Azam Sport 2.
Mchezo huo utachezwa nchini Ethiopia Jumatano ijayo April 18, 2018 ukitarajiwa kuanza saa 10 kamili jioni kwa saa za Tanzania.
Kikosi cha Yanga tayari kimewasili nchini Ethiopia mapema leo.
Ushindi wa nyumbani wa mabao 2-0 unaipa Yanga nafasi ya kutinga hatua ya makundi kama itashinda au kutoka sare kwenye mchezo huo