HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Ijumaa, 13 Aprili 2018

Jeshi la Polisi Mkoani Geita Linamshikilia Mzee wa miaka sitini na tisa (69) kwa kosa la kumuoa Binti wa Miaka kumi na tatu(13)

Jeshi la Polisi Mkoani Geita Linamshikilia Mzee  wa miaka  sitini na tisa (69) kwa kosa la kumuoa Binti wa Miaka kumi na tatu(13)  ambaye anatokea kitongoji cha Rwenge Kijiji cha Bugalama.

Mzee huyo ambaye anajulikana kwa jina la John Mkubila ambaye ni mkazi wa mtaa wa mwembeni kata ya Nyankumbu mjini Geita amekiri kumuoa binti huyo kwa makubaliano ya mzazi  wa binti huyo kuwa awe anamsaidia kazi za nyumbani kutokana na mke wake kuwa na majukumu mengi ya kibiashara hali ambayo imepelekea  kujikuta mzee akikosa huduma za msingi na kuamua kumuoa binti huyo.

“Nilionana na Baba yake nikamwambia kuwa kwa sasa umri wangu umekwenda naweza kupata binti mdogo wa kunisaidia maana kwangu nina mke ila ana majukumu mengi hivyo najikuta nashindwa kufanya shughuli zingine Baba yake akaniambia sawa ndio akawa amenipa huyu ambaye kwa sasa ni Mke Mdogo”Alisema Mzee Mkubila.

Aidha kwa upande wa Binti huyo amekiri kuolewa na mzee huyo  kutokana na  na  Baba yake mzazi kumlazimisha.

“Mimi nilikataa kuolewa Baba yangu ndiye ambaye alinilazimisha niolewe kutokana na kwamba  nimemaliza shule ya msingi ila mimi sikuwa tayari kuolewa kutokana na umri wangu kuwa mdogo”Alisema Binti.

Hata hivyo kwa baadhi ya wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kwenye ofisi za polisi jamii kwenye mtaa huo wamesikitishwa na kitendo hicho na kuitaka jamii kubadilika na kuachana na desturi ambazo zimeendelea kuwakandamiza watoto wa kike .

Kamanda wa Polisi Mkoani Humo Mponjoli Mwabulambo  amesema nyuma ya tukio kulikuwa na mapatano baina ya wazazi wa mtoto na huyo mzee  kama mahari ilitolewa lakini pia uchunguzi unafanyika na utakapokamilika wote watafikishwa mahakamani kwa kuwa ni kosa la kisheria kujamiana na mtoto mwenye  umri wa chini ya miaka kumi na tano(15).