HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 24 Aprili 2018

Kocha mpya Yanga mzuka

Lakini, wakati kocha huyo akitua nchini, straika matata Mnigeria Quadri Kola Aladeokun, ambaye atambadili Donald Ngoma.

SASA ni rasmi George Lwandamina hatarudi kuinoa Yanga na mabingwa hao watetezi bila kupoteza muda wamemshusha kocha matata kutoka DR Congo kuchukua nafasi ya Mzambia huyo. Lakini, wakati kocha huyo akitua nchini, straika matata Mnigeria Quadri Kola Aladeokun, ambaye atambadili Donald Ngoma.

Kwanza, mabosi wa Yanga walitumia saa 48 kusaka suluhu na Lwandamina, ambaye ametimkia kwao akihusishwa na kibarua cha Zesco United na baadaye mambo kukwama wakapiga hesabu za haraka na kufanya uamuzi.

Hesabu zao zikatua kwa haraka kwa Mkongomani Mwinyi Zahera, ambaye yuko kwenye hatua za mwisho kusaini mkataba.

Kocha huyo mpole na asiyependa kuzungumza sana, kwa mara ya kwanza alitua nchini akiwa katika benchi la timu ya DR Congo wakati wakipokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Taifa Stars katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Zahare alitua nchini juzi usiku na kupokewa na msaidizi wa mmoja wa vigogo wazito wa Yanga, ambaye yupo kwenye Kamati ya Mashindano tayari kwa mazungumzo ya mwisho ya kukamilisha mkataba.

Mara baada ya kocha huyo kutua, Mwanaspoti ambalo lilikuwepo uwanjani hapo na kupiga naye stori mbili tatu, alisema amekuja kufanya mazungumzo ya mwisho na Yanga baada ya kuhitaji huduma yake kwa muda mrefu.

Hata hivyo, alisema alishindwa kukubali kibarua cha kujiunga na mabingwa hao wa VPL kutokana na kuwa tayari alikuwa na mkataba na Chama cha Soka cha DR Congo.

Aliahidi kuwa endapo watafikia makubaliano na Yanga basi watarajie kuwa na timu imara na yenye ushindani kwani, anataka kuona timu yake inacheza na watu 10 na sio chini ya hapo.

Akifafanua kauli yake hiyo, Mwinyi alisema jukumu la kwanza litakuwa kutengeneza safu imara ya ulinzi, viungo na washambuliaji ambao kila mmoja atatakiwa kuwa na ujuzi wa kuzuia na kushambulia.

Alisema kikubwa anataka kutengeneza Yanga yenye uwezo mkubwa wa kushambulia na kuzuia vyema, lakini mwisho wa yote Yanga iwe timu yenye kuwapa furaha mashabiki wake.

“Nilikuwa nije hapa zamani, lakini kuna mambo huko nyuma hayakuwa sawa na sikuwa tayari kutokana na kubanwa kimkataba, lakini sasa wameniita tena na nimekuja kumalizia mazungumzo,” alisema Mwinyi.

“Nipo tayari kufanya kazi na Yanga na kuhusu aina ya timu ninayoitaka iwe ni timu ngumu kufungika itakayokuwa na ukuta mzuri, lakini soka langu nataka lichezwe na watu 10 si chini ya hapo. Ukiondoa kipa kila mmoja hapo anatakiwa kujua kuzuia na kushambulia.

Straika Mnigeria yuko nyuma anakuja

Wakati Mwinyi akitua nchini kumalizana na Yanga, ipo katika hatua za mwisho kumleta straika Mnigeria Quadri Kola Aladeokun ambaye ni chaguo la kiungo wa timu hiyo, Pappy Kabamba Tshishimbi.

Kola anakuja Yanga akitokea nchini Swaziland alikocheza pamoja na Tshishimbi wakiwa timu mbili tofauti ambapo, Mnigeria huyo jina lake limepenyezwa kwa mabosi wa Yanga na kiungo huyo, ambaye aliona mapungufu kwenye safu ya ushambuliaji klabuni kwake hapo.

Awali, straika huyo alitarajiwa kutua nchini jana, lakini alikwama na sasa Mwanaspoti linafahamu kuwa atatua mapema wiki hii na atakutana uso kwa macho na Mwinyi kabla ya kuwashauri mabosi wa Yanga kumalizana naye au kumtema.

Yanga inataka kusajili straika wa kigeni atakayechukua nafasi ya Ngoma, ambaye mkataba wake wa miaka miwili aliousauini mwanzo wa msimu ukihesabu siku kutokana na kuchokwa na rekodi zake za majeruhi.

Akili ya Yanga ni kupata straika anayejua kufunga ili kuwasaidia kufanya vizuri kwenye mechi za makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika zinazoanza Mei 6, mwaka huu ambapo vigogo wa klabu hiyo wamepania kuhakikisha wanakuwa na kikosi matata.

Yanga imepangwa Kundi D ikiwa na klabu za USM Alger (Algeria), Gor Mahia (Kenya) na Rayon Sport (Rwanda) na imeapa kuwa safari hii ni lazima ifike mbali tofauti na misimu mingine.