Jana Aprili 14, 2018 Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilipata Rais mpya mteule Bi. Fatma Karume, Hatimaye Mhe. Tundu Lissu ambaye ndiye aliyemuachia kiti hicho ametoa pongezi kwa wanachama wa TLS.
Mhe. Tundu Lissu
Mhe. Lissu ambaye yupo hospitalini nchini Ubelgiji tangu mwezi Januari mwaka huu, amesema kuwa uchaguzi huo umethibitisha kuwa TLS ni chama ambacho kinaweza kujisimamia na kujiendesha bila kuingiliwa na mtu.
“Napenda kuwapongeza wanachama wote wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kwa kumchagua Bi. Fatma Karume kuwa Rais mpya wa TLS. Uchaguzi huu umethibitisha, kwa mara nyingine tena, umuhimu wa Chama cha kitaaluma cha mawakili kujisimamia na kujiendesha bila kuingiliwa,“ameeleza Tundu Lissu na kutoa pongezi kwa Bi. Fatma .
“Namtakia Rais Mteule Fatma Karume kila kheri katika kutelekeza majukumu yake mapya na muhimu katika kipindi hiki cha historia ya nchi yetu.“ameandika Mhe. Lissu kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Wakili Fatma Karume amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) jana mjini Arusha kwa ushindi wa kura 820 akiwamwaga Godwin Ngwilimi kura 363, Godwin Mwapongo 12 na Godfrey Wasonga kura 6.