Habari:Waziri wa nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Willium Lukuvi amesema kero wanayopata wapangaji wa nyumba kulazimishwa kulipa kodi ya mwaka mzima ama miezi sita kwa mkupuo itafikia tamati siku chache zijazo.
Waziri Lukuvi amesema hayo mkoani Dodoma wakati akifungua maoenesho yanayohusiana na ujenzi wa nyumba na umiliki ardhi yanayoendelea katika viwanja vya Bunge na kusema Serikali ipo katika hatua za mwisho kuunda chombo maalum cha kusimamia sekta ya nyumba.