FIDIA KWA WAFANYAKAZI: Serikali imesema inafanya tathimini ili kupitia upya sheria ya viwango vya fidia kwa wafanyakazi baada ya kupokea malalamiko kutokana na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyazi kulipa kiwango kidogo.
Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu, Jenista Mhagama wakati akizungumza na waajilri wa sekta binafsi ambapo amesema wakati serikali ikiendelea kupitia upya sheria hiyo, wafanyakazi wanatakiwa kujiunga na mfuko huo wa fidia ili waweze kunufaika pindi wanapokuta na matatizo.