HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 9 Aprili 2018

Kuelekea mchezo Wa Mtibwa Vs Simba

Kuelekea kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara baina ya Simba SC dhidi ya Mtibwa Sugar utakao pigwa jioni ya leo uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Afisa habari wa wana tam tam, Thobias Kifaru ametamba kuwafundisha adabu vinara hao wa ligi na kuahidi kuzitia dosari mbio zao za kutwaa ubingwa msimu huu.

Akizungumza kwenye kipindi cha michezo cha Magic Fm, Kifaru ‘Ligalambwike’ amesema kuwa wamejipanga kuvunja ngome za Simba SC kama walivyofanya hivyo kwa Azam FC kwenye michuano ya kombe la Shirikisho.

Tutatumia uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa sababu Simba SC ni timu kubwa ni kama tunavyokutana na Yanga SC pia huwa tunatumia dimba hilo, hizi ni timu kongwe na zinamashabiki wengi kwa hiyo ni lazima kutumia hapo.

Tutanyatia nyatia tutie dosari mbio zao za kuwania ubingwa wa ligi kuu, tutabomoa ngome za Simba SC watanisamehe kwa hili. Wao ni wakawaida sana wana mikono miwili na miguu miwili na wahasa mashabiki wajitokeze kwa wingi.


Kuelekea kwenye mchezo huo Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji kwa kuwakaribisha Simba SC  wakati timu zote hizi zikiwa na kumbukumbu ya kufanya vizuri kwenye michezo yao iliyopita ambapo Wana tam tam Mtibwa wakiifunga Singida United jumla ya mabao 3 – 0 huku mnyama Simba ikiibuka na ushindi 2 – 0 dhidi ya Njombe Mji FC.