Kuondoka kwa Lwandamina kumeiathili yanga
Yanga iliingia kucheza mechi ya VPL dhidi ya Singida United bila kocha wake mkuu George Lwandamina ambaye ametimki ZESCO United ya Zambia, bechi la ufundi la Yanga katika mchezo huo liliongozwa na kocha msaidizi Shadrack Nsajigwa.
Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya kufungana 1-1, mara baada ya kumalizika mchezo huo Nsajigwa alizungumza na waandishi wa habari kuelezea kwa ufundi mchezo ulivyokua. Nsajigwa amekiri kwamba matokeo ya sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Singida huenda yamechangiwa na kutokuwepo kwa kocha mkuu kwenye benchi la ufundi.
“Hata kwenye familia mmoja wenu akipungua ambaye alikuwepo kwa mfano baba lazima kuna vitu havitakuwa sawa”-Shadrack Nsajigwa, kocha msaidizi Yanga.