HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Alhamisi, 12 Aprili 2018

Makala: Nafasi ya waandishi wa habari na wananchi katika kupambana na rushwa

Makala: Nafasi ya waandishi wa habari na wananchi katika kupambana na rushwa
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hivi karibuni alizungumza kuhusu ukwepaji kodi na kuvipa vyombo vya habari kazi kubwa ya kuwatafuta popote walipo watu wanaokwepa kodi na kuwaweka bayana.

Wakati akitoa wito huo, Charles Kicheere aliwaweka wananchi na vyombo vya habari katika wakati mgumu wa kutekeleza jukumu hilo kubwa la kuwatafuta na kuwatangaza wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na ukwepaji kodi. Hii ina maana kuwa, TRA inahitaji msaada kuweza kuwapata watu hawa kwani wamo ndani ya jamii.
TRA hawawezi kufanya kazi hii wenyewe, na pia anawakumbusha wananchi kuwa kupambana na rushwa na wakwepaji kodi ni jambo muhimu katika kuhakikisha taifa kwa pamoja linafanikiwa.

Je! Waandishi wa habari wamejibu ombi hili? Jibu ni kwamba, bado. Au tunaweza kusema hawajajibu ombi ili katika kiwango chenye mashiko.
Ni vigumu kusema kwamba, tangu ombi hilo lilipotolewa kuna mwandishi wa habari yeyote aliyetembelea ofisi za TRA au TAKUKURU na kutoa taarifa kuhusu vitendo vya rushwa au ukwepaji kodi  au ambaye ameivalia njuga habari ya kiuchunguzi na kuiibua.
Kuna uoga au watu hawako tu tayari kufanya hivyo? Utafiti hivi karibuni ulifanywa kuangalia ni kwa kiasi gani wananchi wapo tayari kutoa ushahidi au kutoa taarifa kuhusu matukio ya rushwa, matokeo ya utafiti huo yanakatisha tamaa kusoma.
Watu wengi wamekuwa wakihofia kuhusu usalama wao pale wanapotaka kutoa taarifa kuhusu vitendo vya rushwa, wakiamini kwamba watakapotoa taarifa hizo, watuhumiwa hao watawadhuru.

Ni imani ya serikali kuwa, waandishi wa habari watajiona wako salama kiasi kwamba watakuwa huru kuzungumzia mambo haya yanayovunja sheria za nchi.
Matokeo ya kazi yao hayataweza kuonekana au kupimwa hadi pale taarifa za wala rushwa zitakaporushwa na vyombo vya habari na kuwa katika kurasa za mbele za magazeti.

DOWNLOAD KATISHA BLOG APP BONYEZA HAPA CHINI

KATISHA BLOG

KATISHA BLOG
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD KATISHA BLOG APP IN GOOGLE PLAY STORE ...ANDIKA KATISHA ...SEARCH