HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 28 Aprili 2018

Kwa Mkongomani huyu, Simba lazima wajipange


Na.mwanaspoti.co.tz

Yanga iliyojichimbia kambini mjini hapa huku jioni ya juzi Jumatano ikimpokea Kocha Mkuu wake mpya, Zahera Mwinyi kutoka DR Congo, imepania mchezo huo na kama vijana hao wa Jangwani watazingatia maelekezo na mbinu za Mkongomani wao, mambo lazima yajipe.

ACHANA na presha kubwa waliyonayo wadau wa Yanga mjini hapa kiasi cha kuweka ulinzi mkali na kuzuia hata waandishi wa habari wasifanye kazi yao kwa uhuru, lakini ukweli ni kwamba Simba lazima ijipange Jumapili itakapovaana na vijana hao wa Jangwani.

Yanga iliyojichimbia kambini mjini hapa huku jioni ya juzi Jumatano ikimpokea Kocha Mkuu wake mpya, Zahera Mwinyi kutoka DR Congo, imepania mchezo huo na kama vijana hao wa Jangwani watazingatia maelekezo na mbinu za Mkongomani wao, mambo lazima yajipe.

Zahera anayemudu kuzungumza lugha za Kifaransa, Kiingereza na Kiswahili, ile kutua tu kambini hiyo juzi alianza kazi yake kwa kishindo akitumia saa mbili kuwacheki wachezaji na kutoa maelekezo kwa Kocha Msaidizi, Shadrack Nsajigwa, ili kuweka mambo sawa.

Mwanaspoti ambayo imepiga kambi mjini hapa kuwachabo Yanga na wapinzani wao Simba ambao mchana wa jana Alhamisi walianza safari ya kurudi Dar na leo Ijumaa watajifua Uwanja wa Boko Veterani, ilimshuhudia kocha huyo akiwalazimisha vijana wake kupiga mpira mwingi akitumia neno kabumbu na kuwavunja mbavu mashabiki.

Kwanza Zahera alipata wakati mgumu kuwatambua wachezaji wake uwanjani kutokana na kuwa ni mara yake ya kwanza kuwa nao, lakini alionekana kufurahia kile walichokuwa wakikifanya katika kila zoezi alilokuwa akiwapa.

Unajua alianzaje? Mara baada ya kutua kwenye mazoezi hayo yanayofanyikia Uwanja wa Highland, kocha Zahera aliwapangia koni wachezaji na kuwataka wakimbie kwa kasi huku wakizizunguka koni hizo kwa nyuma na aliwagawa makundi mawili, huku akitaka kila kundi kusiwe na mchezaji anayetegea.

Baada ya kumaliza zoezi hilo aliwataka wachezaji wacheze soka la chini katika zoezi lililosimamiwa kwa umakini na benchi la ufundi.

Zahera akisaidiana na David Mwandila na Nsajigwa, waligawa timu mbili na kuwataka wakipige huku wakiwasisitiza wacheze mpira kwa pasi mbili mpaka tatu.

Yanga ilionekana kutotaka kukaa na mpira hata kidogo, mchezaji ambaye alikuwa akikaa na mpira makocha walikuwa wakali dhidi yake.

Baada ya Zahera kuwa uwanjani na wachezaji wake kwa muda huo wa zaidi ya dakika 120, alionekana kutaka kumfahamu vizuri kila mchezaji hasa katika uchezaji wao baada ya kuwasoma kwa umakini.

Hata hivyo wachezaji nao walionekana kuwa na furaha na morali muda wote katika mazoezi hayo, baada ya kukosekana kwa aliyekuwa Kocha Mkuu George Lwandamina aliyerejea kwao Zambia kinyemela.

Kwa kazi iliyofanywa na Zahera juzi, iliwafanya mashabiki waliokuwapo uwanjani hapo kuamini kuwa Jumapili Simba lazima iteme pointi tatu.

Mabosi wa Yanga wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika na mjumbe wake Salum Mkemi, walifika mazoezini hapo wakati Zahera akifanya yake.

Nyika alisema uwepo wao ni kuwapa motisha vijana wao kuelekea katika mchezo wa Jumapili.

“Motisha ipo lakini hatuwezi kuiweka wazi kwa sasa, kama ulivyotuona tulianza kufika hotelini na kuzungumza na vijana na wamehamasika,” alisema.

Nyika aliongeza kwamba kufika kwa kocha Zahera, kumeongeza morali pia.