MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita zimesababisha mafuriko aktika maeneo mbalimbali ya jiji huku watu kadhaa wakiripotiwa kufariki dunia kutokana na mvua hizo.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi, Lazaro Mambosasa amesema amepokea taarifa ya watu tisa kufariki dunia kutokana na mvua hizo huku wengine wakijeruhiwa.
Kamanda Mambosasa amesema vifo hivyo vimetokana na kuangukiwa na ukuta na wengine kusombwa na maji kutokana na mvua zilizonyesha kwa siku tatu mfululizo.
Mambosasa amesema mwili mmoja uliosombwa na mafuriko umekutwa ukielea majini kuelekea eneo la Jangwani.


