HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatano, 11 Aprili 2018

Majaji wawili wajiuzulu

Majaji wawili wajiuzulu


Majaji wawili wa Mahakama ya Katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamejiuzulu kwenye nafasi zao, na kusalia majaji sita badala ya tisa katika Mahakama hiyo.

Jaji mmoja alifariki dunia siku ya Jumapili na wengine wawili wamejiuzulu bila hata  kutoa maelezo au sababu ya kujuzulu kwao.

Majaji hao ambao ni  Jean-Louis Esambo na Banyaku Luape wamedaiwa kutoripoti katika Mahakama ya Katiba, Mnamo Oktoba 17, 2016, ambayo ingetoa uamuzi muhimu kuhusu hatma ya DRC.

Imeelezwa kwamba Tangazo hilo limeishangaza serikali ya DRC kwa uamuzi  huo ingawa majaji hao wawili walionesha zaidi ya mara moja maoni tofauti na rais wa mahakama hiyo.