MAHOJIANO MAALUM: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pia ametoa ufafanuzi wa namna ambavyo zoezi hilo linavyofanyika, baada ya kuulizwa iwapo Baba mtuhumiwa atakataa wito kwa madai mtoto siyo wa kwake.
"Tunachofanya, ni kukusikiliza baada ya kupokea malalamiko ya mwanamke aliyekutaja, ila kama utakataa hatua za kisheria zitachukuliwa. Sasa kama unakataa wito sisi tutasikilizaji utetezi wako." Paul Makonda.
SWALI: Na kama mtu atabainika kuwa mtoto siyo wa kwake baada ya vipimo vya DNA hatua gani zitachukuliwa? kutokana na ukweli kuwa wapo watu wamepanga kwenda kukushtaki kwa kuwadhalilisha?
MAKONDA: Kila kosa liko kisheria kama ilivyo kosa la kukaidi wito wa kiongozi wa serikali, ndivyo itakavyokuwa kwa mama aliyedanganya, kwani kwa atakayebainika kumbambikia mwanaume mtoto kwa mujibu wa vipimo atashtakiwa kwa kosa la kudanyanya mamlaka.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema yeye amefanya zoezi hilo kwa lengo la kuwataka wazazi hao kuwajibika kwa mtoto husika.
Amesema mtoto ana haki ya kulindwa, kupewa matunzo na kutumia jina la Baba yake.
Pia amesema, amesikia kashfa nyingi kuhusu zoezi hilo lakini anachoamini ni kuwa ni suala jema kwake mbele ya Muumba wake na kwa mtoto.
"Hawa wamama mimi kwangu ni mashujaa kwangu, wamekuwa wakihangaika na kuteseka na watoto pekee yao."