Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imewataka wakazi wa mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba kuchukua tahadhari kutokana na matarajio ya uwepo wa mvua kubwa inayozidi milimita 50, kuanzia usiku wa leo Aprili 13.