HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 16 Aprili 2018

Msuva azidi kutupia mabao El jaddidi


STRAIKA wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya Difaa Hassan El Jadidi, Simon Msuva ameendelea kuwa lulu kwa mashabiki wa timu hiyo na kwamba wasipomuona uwanjani nafsi zao zinakosa amani.

Msuva amekuwa mchezaji muhimu sana ndani ya kikosi hicho ambapo taarifa kutoka Morocco zinasema si mashabiki tu wanaomkubali bali hata wachezaji wenzake wamekuwa wakivutiwa sana na uwezo anaouonyesha na kuisaidia timu mara kwa mara.

Hali hiyo imezidi kuthibitika baada ya hapo jana kuinusuru timu yake kutoka kwenye kichapo akiitoa nyuma kwa mabao 3-1 na kuifungia mawili yaliyoifanya ipate sare ya mabao matatu ugenini dhidi ya Olympique Khouribga.

Mabao hayo mawili katika dimba la Stade du Phosphate yamemfanya Msuva afikishe jumla ya mabao manane kwenye ligi kuu nchini Morocco maarufu kama Botola ambapo mwenyewe amekiri suala la kuendelea kukubalika nchini humo.

“Ni kweli kabisa ulivyoambiwa, mashabiki wanakubali kazi ninayofanya huku na wanaheshimu sana uwezo wangu,” alisema Msuva.


Jadidi inayotarajiwa kucheza na Raja Casablanca Aprili 22 wamejiongezea pointi moja na kufikisha 38 wakiendelea kusalia katika nafasi ya nne nyuma ya vinara IR Tanger wenye 47 (kabla ya mechi yao dhidi ya FUS Rabat), HUSA (41) na OC Safi wenye 39.