HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 23 Aprili 2018

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI AJIUA BAADA KUBAINI ANAISHI NA VVU


Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mwasele iliyopo katika manispaa ya Shinyanga Happiness William (18) amefariki dunia kwa kujinyonga kwa kwa kutumia kamba kutokana na msongo wa mawazo baada ya kubaini kuwa anaishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU). 

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule tukio hilo limetokea jana Aprili 22,2018 majira ya saa 12 na dakika 40 jioni. 

Alisema mwanafunzi huyo,mkazi wa Kambarage mjini Shinyanga aligundulika akiwa amefariki baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba aliyoifunga kwenye paa la nyumba aliyokuwa anaishi na wazazi wake. 

“Chanzo cha tukio ni msongo wa mawazobaada ya kugundua kuwa anaishi namaambukizi ya VVU,mwili wa marehemuumefanyiwa uchunguzi wa daktari nakukabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili yamazishi”,alieleza Kamanda Haule. 

Aidha alitoa wito kwa wazazi,walezi na wananchi kwa ujumla kuwa karibu na watoto na vijana ili kujua shida na changamoto zinazowakabili ili kuchukua hatua za kuwashauri na kuwatia moyo wa matumaini pale wanapokata tamaa ya maisha.