HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 28 Aprili 2018

PROFESA LIPUMBA AZUA TAHARUKI BUNGENI 

Gabriel Mushi, Dodoma

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba leo amezua taharuki bungeni kwa muda wa dakika moja baada ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumshangilia.

Wabunge hao wa CCM  walianza kumshangilia pindi alipotambulishwa bungeni jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Bunge, Musa Hassan Zungu kama mmoja wa wageni waliowasili bungeni siku ya leo.

Aidha, kutokana na utambulisho huo wabunge wa CCM walimshangilia kwa nguvu huku wakisema ‘kiboko yao’ wakati wabunge wa vyama vya  upinzani nao wakimshangilia na kusema: ‘CCM.. CCM’.

Hali hiyo ilimlazimu Zungu kuwakemea wabunge hao kukaa kimya kwani muda wanaotumia kumshangilia unatakiwa kutumika katika kuchangia hotuba za bajeti.

Bajeti zinazotarajiwa kuwasilishwa leo ni za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.