HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 28 Aprili 2018

Wasanii watabiri mshindi mechi ya Simba, Yanga kesho


Zimebaki saa chache kabla ya pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga kufanyika kesho Aprili 29 jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara umekuwa ukitawaliwa na tambo za mashabiki wa timu hizo, kila upande ukitamba kutoka uwanjani na ushindi.

Katika ushabiki huo,wasanii wa filamu na muziki nao hawajabaki nyuma kwani wameonekana kutoficha hisia zao kuelekea katika mpambano huo.

Mwigizaji Mboto amesema atakuwa miongoni mwa mashabiki watakaowahi uwanjani hapo na kuisapoti timu yake ya Yanga.

“Simba watarajie kipigo tu kwetu, wanaona kama wana kikosi bora lakini nawakumbusha tu wasijisahaulishe kama vile hawawajui  Yanga wanavyowaliza na wajue kuongoza ligi si kuifunga Yanga. Simba wategemee kipigo cha bao 3-1 kwa mchezaji yeyote wa Yanga kwani wote nawaamini wako vizuri, tena hili bao lao moja nililowapa litakuwa la kusafishia njia tu."

Mwana FA ambaye ni shabiki wa Simba anasema hawawezi kupoteza ndoto za ubingwa kwa kufungwa na Yanga.

"Nakiamini kikosi cha Simba sababu kipo imara na kina wachezaji wenye uwezo mkubwa, hivyo sitegemei kupoteza ndoto za ubingwa kwa kufungwa na Yanga, yaani Yanga wategemee mabao mawili kwa Kichuya na Okwi."

Irene Uwoya

Staa huyo wa Bongo Movie ambaye ni shabiki wa Yanga amekihakikishia ushindi kikosi chake na kudai kitaifunga Simba goli 3-1 na magoli hayo yatafungwa na Ibrahim Ajibu,Chirwa na Hamis Tambwe.

Snura Mushi  amekuwa na mahaba makubwa na Simba akisema kutokana na kiwango kizuri cha wachezaji wa Simba ni dhahiri ubingwa kwao hauzuiliki na anategemea magoli mawili kutoka kwa Kichuya.

Mwigizaji Jacob Steven ‘JB’ anasema chama lake Simba litatoa kichapo kwa watani wao hivyo wakae mguu sawa.

Anasema Simba iko imara kuanzia wachezaji, benchi la ufundi hadi mashabiki hivyo haoni kitakachowazuia kuchukua ushindi wa bao tatu kutoka kwa Kichuya, Okwi na Niyonzima.

Wema Sepetu

Wema ambaye ni shabiki wa Yanga amesema amekuwa na mapenzi makubwa na timu hiyo tangu akiwa mdogo na ataendelea kuisapoti itakapocheza mechi ya aina yoyote, ila kwa mpambano huu wa Jumapili ataitabiria Yanga ushindi wa bao 1-0 kwani anaona Simba nao wamekuja vizuri katika ligi.

"Mimi ni shabiki mzuri tu wa Yanga na nategemea timu yangu kuifunga Simba goli moja tu bila, maana naona nao wamekuja vizuri japo hawatasumbua sana uwanjani. Tuwaachie Yondani na Ajibu wafanye yao.”

Madee Ali ambaye ni shabiki wa Simba, amesema Yanga italizwa goli 2-0 na mchezaji waliyekuwa wanadai ni mzee Emmanuel Okwi.

"Dada yangu unauliza nani kushinda katika mpambano huu wakati inajulikana, ni ushindi wa Simba jamani, jua kabisa yule mchezaji mzee ndio atawaliza Yanga kwa bao moja kwa bila.