Baada ya kutokea hali ya taharuki na malalamiko kwenye mchezo uliyochezwa mwishoni mwa juma lilioisha kati ya Mbeya City na Yanga, leo hii uongozi wa Mbeya City umeibuka na kudai mambo yanayozunguzwa na baadhi ya watu ni tofauti kabisa na hali halisi jinsi ilivyokuwa uwanjani.

Hayo yameelezwa na Mtendaji wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe wakati alivyokuwa anazungumza na waandishi wa habari baada ya kupita siku kadhaa tokea wapinzani wao Yanga kutoa malalamiko kuwa walichezesha wachezaji 11 uwanjani badala ya 10 kama inavyotakiwa kuwa.
"Mwamuzi Shomary Lawi hakuutendea haki mchezo wetu kwenye hili tupo 'very clear' na kwa bahati mbaya sio mara ya kwanza kuharibu mchezo wetu. Mwamuzi alikataa penati ya wazi baada ya mpira kuzuiliwa kwa mkono na Gadiel Michael, hata Gadiel kwa lugha ya picha alikubali ile ilikuwa ni faulo", amesema Kimbe.
Pamoja na hayo, Kimbe ameendelea kwa kusema "hatuwakatazi Yanga kukata rufaa kwa sababu ni haki yao ila waiache mamlaka husika ifanye uchunguzi wake na kutoa maamuzi sahihi nasio kuwaendesha kutoa maamuzi, hakuwa na mchezaji aliyepewa kadi na akarudi uwanjani, hatukucheza wachezaji 12".
Kwa upande mwingine, Kimbe amesema mchezaji wao Ambokile ambaye analalamikiwa juu ya tukio hilo kuwa alikaa uwanjani kwa sekunde 42 kisha akatoka uwanjani baada ya kuambiwa kwamba amefanyiwa mabadiliko nasio kuwa aliendelea kucheza kabumbu.
INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO upate habari kwa haraka zaidi
bonyeza hapa chini