HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatano, 11 Aprili 2018

Sakata la Wanawake Waliotelekezwa na Watoto na Wabunge Lamfikia Ndugai Ataka Wapeleke Vyeti Kupima DNA

Sakata la Wanawake Waliotelekezwa na Watoto na Wabunge Lamfikia Ndugai Ataka Wapeleke Vyeti Kupima DNA



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema zoezi linaloendelea katika Mkoa wa Dar es Salaam linaloongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda, la kuwatafutia haki wanawake waliowatelekezewaa watoto na wanaume waliozaa nao bila kuwahudumia na halikadhalika wanawake waliowakimbia wanaume zao na kuwaacha na watoto limemtikisa. 

Spika Ndugai amesema baada ya Makonda kukutana na akina mama hao ambapo inadaiwa wapo baadhi ya Wabunge waliotajwa kutelekeza watoto.

Ndugai amesema (kwa utani) amesikia wapo na wanaume walitelekezewa watoto na akina mama ambao ni wabunge huku

akiwaomba wamuandikie barua na wamletee cheti kinachoonyesha na kuthibitisha Kipimo cha Vinasaba vya uzazi ‘DNA’.