Pichani ni mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC)Geffrey Mwambe akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka nchini Ujelumani ambapo wameonesha nia ya kuja kuwekeza nchi(hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam, NA KAROLI VINSENT
KITUO cha Uwekezaji nchini (TIC) imeziomba Taasisi zote za Serikali kuhakikisha wanarekebisha huduma wanazotoa kwa kuhakikisha wanatoa huduma kwa haraka kwa Wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar Es Salaam na Mkurugenzi wa (TIC) Geffrey Mwambe,wakati akizungumza na waaandishi wa Habari mara baada ya kumalizika Kikao kati ya Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka nchini Ujelumani ambapo wameonesha nia ya kuja kuwekeza nchi.
Amesema ni wakati wa Taasisi za Serikali zinazotoa huduma ikiwemo zile zinazotoa Hati za kusafiria,zinazotoa viwanja ,Viza,Vibali vya Mazingira,kuhukakisha wanatoa huduma kwa Wawekezaji kwa haraka.
“Naziomba Taasisi za Serikali zirekebisha huduma wanazotoa kwa wawekezaji,kwani hawa Wawekezaji wanaokuja nchini wanakuwa ni mabarozi kwa Wawekezaji wenzao huko kwao,nazisihi Taasisi hizi kutoa huduma kwa kiwango cha haraka ili tuweze kuwavutia Wawekezaji wengi”Amesema Mwambe.
Amesema Ujio wa Wawekezaji hao kutoka Ujelumani utafungua Fursa kwa nchi pamoja kuwainua wakezaji wa ndani.
“Hawa wanakuja hapa watashirikiana na sekta Binafsi katika kufanya kazi kwenye miradi yao mbali mbali ambapo watasaidia kukuza Sekta binafsi,wafanyabiashara wetu tuhakikishe tunatumia fursa ujio wa hawa wenzetu katika kuinuka ,hawa wanapenda kushirikiana na kampuni ya ndani kwani kampuni za ndani wanakuwa na uzoefu wa hapa nchini,”Ameongeza kusema Mwambe
.
Aidha,Mwambe amesema ujio wa wafanyabiashara hao kuja kuwekeza nchini utakuwa ni wafaida mkubwa ndani ya nchini,kwa kuweza kusaidia kuongeza ajira pamoja na kukuza Teknolojia.
Hata Hivyo,Mwambe amebainisha kuwa sababu iliowafanya wawekezaji hao kuchagua kuja kuwekeza nchini imetokana na hali nzuri ya uwekezaji nchini ikiwemo hatua alizochukua Rais John Magufuli katika kushughulikia suala la Rushwa
Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka nchini Ujelumani wakimsikiliza kwa Makini Mkurugenzi wa TIC ,
Kwa upande wake Dkt Janes Follhabe ambaye ni kiongozi wa wafanyabiashara hao amesema wamefurahishwa na mazingira ya uwekezaj nchi kuwa mazuri na rafiki kwa uwekezaji