HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Alhamisi, 26 Aprili 2018

Tambwe afanya mazoezi na Yanga Morogoro

Mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe anajifua kikamilifu kuelekea mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba Jumapili ijayo.
Tambwe ameungana na kikosi cha Yanga mkoani Morogoro baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City.
Amekuwa akifanya mazoezi ya timu kikamilifu na mazoezi mengine ya ziada ili kuhakikisha anapata 'match fitnes' haraka.

Yanga inakabiliwa na michezo 13, saba ya ligi na sita ya kombe la Shirikisho hivyo kurejea kwake kutaongeza nguvu.
Pia Yanga itashiriki mashindano ya Sportpesa yatakayoanza mwanzoni mwa mwezi wa sita ambapo mwaka huu yatahusisha timu kutoka Tanzania, Kenya na Afrika ya Kusini
Mbali na Tambwe, beki Andrew Vicent na mshambuliaji Ibrahim Ajib nao waliungana na kikosi cha Yanga mkoani Morogoro.

Habari njema zaidi ni kupona kwa kiungo Papi Tshishimbi.
Tshishimbi alikosa mazoezi ya siku ya kwanza sambamba na Obrey chirwa, lakini wote tayari wamewasili mkoani Morogoro na leo wameshiriki mazoezi ya asubuhi kikamilifu.
Kelvin Yondani aliyetolewa wakati wa mapumziko kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City baada ya kuumia kifundo cha mguu, ni miongoni mwa wachezaji wanaojifua kikamilifu na kikosi cha Yanga 
Tayari kocha mpya wa Yanga, Mwinyi Zahera amewasili mkoani Morogoro na jioni hii ya Jumatano wakati wa mazoezi, atakutana na wachezaji pamoja na benchi la Ufundi.

INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO upate habari kwa haraka zaidi

             bonyeza hapa chini
INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD KATISHA BLOG APP IN GOOGLE PLAY STORE ...ANDIKA KATISHA ...SEARCH