HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Ijumaa, 20 Aprili 2018

Ushauri kwa yanga

Mdau wa klabu ya Yanga Steve Kampira pamoja na beki wa zamani wa timu hiyo Keneth Pius Mkapa wamesema Yanga inahitaji kujiimarisha zaidi kwenye nafasi kiungo na ushambuliaji ili ifanye vizuri kwenye michuano ya kombe la Shirikisho hatua ya makundi.

Pichani Kenneth Mkapa enzi zake akiwa na Marehemu Said Mwamba, mwaka 1993

Yanga imetinga hatua ya makundi baada ya kuiondoa Wolaitta Dicha kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 licha ya kufungwa bao 1-0 nchini Ethiopia juzi.

Akizungumza katika kipindi cha Yanga TV, Mkapa amesema hana mashaka na safu ya ulinzi ya Yanga lakini ni dhahiri kunahitajika uwekezaji zaidi katika nafasi ya kiungo na ushambuliaji.

Amesema katika mchezo dhidi ya Dicha Yanga ilikosa muunganiko mzuri kutoka kwenye kiungo na ushambuliaji.

Amesema si vibaya kama Yanga itasajili kiungo mwenye uwezo zaidi wa kulisha mipira kwa washambuliaji.

Naye Kampira amemkosoa kiungo Pius Buswita na kumtaka abadili aina yake ya uchezaji ili aweze kuisaidia zaidi timu.

"Katika mchezo dhidi ya Dicha, kuna wakati Chirwa alikuwa peke yake mbele akikabwa na watu wanne, Buswita alitakiwa kusaidiana nae"

"Buswita ni mchezaji mzuri lakini inabidi aache utoto ili aweze kudhihirisha ubora wake"

Kuelekea hatua ya makundi Yanga ina nafasi ya kusajili mchezaji/wachezaji kukamilisha idadi ya wachezaji 30 kama orodha ya awali iliyotumwa CAF mwezi Januari ni pungufu ya wachezaji hao.