HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatano, 18 Aprili 2018

Waandishi wamsaka ajibu Ethiopia

Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini Ethiopia wamefika hoteli ya Rori ilipoweka kambi klabu ya Yanga wakitaka kufanya mahojiano na kiungo mshambuliaji, fundi Ibrahim Ajib Migomba.

Kiwango alichoonyesha kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 kimewafanya 'Ma-ras' hao wapagawe.

Ajib ameachwa jijini Dar es salaam kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Singida United.

Leo saa kumi kamili jioni Yanga inashuka kwenye uwanja wa Hawassa kuikabili Wolaitta Dicha kwenye mchezo wa marudiano wa kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho.

Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo. Hakuna majeruhi na amewataka Watanzania kuiombea dua Yanga ili iweze kuiwakilisha vyema nchi.