Rapa Billnass ambaye anatamba na ngoma ya 'Tagi Ubavu' amefunguka na kuweka wazi kwa jamii kuwa Alikiba ni miongoni mwa wasanii ambaye anampa ushirikiano mkubwa kwa kila jambo ambalo huwa analifanya katika harakati zake na kudai siku zikikaribia huenda wakatoa wimbo wa pamoja.
Billnass ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa kijamii wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia majira ya saa 8:00 mchana hadi 10:00 jioni baada ya kuonekana picha katika mitandao za kijamii zikiwaonesha wawili hao wakiwa studio katika siku za nyuma kidogo.