HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Ijumaa, 13 Aprili 2018

Wakala :Neymar hawezi kucheza pamoja Ronaldo

 Wakala :Neymar hawezi kucheza pamoja Ronaldo

WAKALA maarufu wa soka, Pini Zahavi amesema haoni uwezekano wa Neymar kuhamia Real Madrid wakati Cristiano Ronaldo akiwa klabuni hapo akisisitiza kuwa kuna nafasi moja tu ya ‘Supastaa’ kwenye kila timu.

Mtandao wa Soccernetreports umeripoti kuwa Zahavi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na gazeti la Przeglad Sportowy la nchini Poland huku akimtaja mteja wake mpya, Robert Lewandowski kuwa ndiye straika bora zaidi kwasasa hapa duniani akielezea taarifa za mwezi uliopita zilizodai mfumania nyavu huyo wa Bayern Munich amefikia makubaliano ya kutua Madrid.

Zahavi, ambaye alikuwa dalali katika mchakato wa Roman Abramovich kuinunua Chelsea na uhamisho wa rekodi wa Rio Ferdinand kutua Manchester United, alisimamia vema uhamisho wa Neymar kutoka Barcelona kwenda PSG.

Ronaldo akiwa na Messi katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya uliozikutanisha Real Madrid na PSG

Kwa mujibu wa UOL Esporte, wakala huyo raia wa Israeli aliongozana na vigogo wa PSG mwezi uliopita kwenda Brazil kutazama maendeleo ya afya ya Neymar na kutathmini thamani ya nyota huyo kwenye dirisha lijalo la usajili baada ya taarifa kuvuja kuwa hana furaha jijini Paris.

Zahavi aliiambia Przeglad Sportowy kuwa Neymar alilazimika kuondoka Barcelona ili kukwepa ‘kivuli’ cha Messi kwavile ni ngumu kwa klabu moja kuwa na nyota zaidi ya mmoja kati ya wale watatu bora hapa duniani (Ronaldo, Messi na Neymar).

“Neymar alifanya kitu ambacho alipaswa kukifanya kwa wakati ule. Kuna masupastaa watatu tu kwenye soka ambao ni Ronaldo, Messi na Neymar, hawa hawawezi kucheza klabu moja.


Neymar akifurahia jambo na Messi wakati akiitumikia Barcelona kabla hajatimkia PSG

 

“Pale Barca, Neymar alilazimika kuwa namba mbili, namba mbili katika upigaji wa adhabu ndogo, namba mbili kwenye kupiga penati, kwa kifupi alikuwa namba mbili kwa kila jambo.” Alisema Zahavi.


Wakala huyo alimaliza kwa kusema Neymar aliwasili Hispania akiwa kijana mdogo lakini sasa amekua, ana miaka 26 hivyo ana miaka kama minane au tisa tu ya kukaa kileleni jambo ambalo linamfanya ahitaji uhuru zaidi.