HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 28 Aprili 2018

Wakenya 'wamkataa Rick Ross' wakidai aliyewasili Kenya si yeye, hii hapa sababu


-Wakenya mitandaoni wameikashifu NRG Wave Concert wakisema walimleta nchini Rick Ross feki

-Wengi walitarajia kumuona msanii huyo wa Merikani kwa mwili wake wa miraba minne

-Alipowasili katika uwanja wa ndege, alikuwa na mwili wa kawaida suala lilowafanya Wakenya kujua kuwa ‘walichezwa’

Msanii maarufu wa nyimbo za kufoka raia wa Amerikani Rick Ross alitua katika uwanja wa ndege wa JKIA tayari kuwatumbuiza Wakenya katika hafla iliyondaliwa na NRG Wave concert.

Kama ilivyoripotiwa na jarida la TUKO.co.ke, Rick Ross anatarajiwa kupiga shoo Jumamosi, Aprili 28 katika kilabu ya Cannivore, Nairobi.

Wakenya wadai aliyewasili nchini ni Rick Ross feki

Kilichowashangaza wengi ni kuwa Rick Ross waliyemuona akitua katika uwanja wa JKIA siye wanayemjua. Msanii huyo anajulikana kuwa na mizani kibao na haswa tumbo lake ambalo kwa kawaida ‘linaanguka’.

Suala hili liliibua hisia mseto huku wengi wakidai kuwa waandalizi wa hafla hiyo waliwalaghai mashabiki fedha na kumleta nchini Rick Ross feki.

Jaridala TUKO.co.ke limetbitisha kuwa huyo ndiye Rick Ross asili ila alifanya mazoezi na kupunguza uzani wake kwa kiwango kikubwa.