HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 16 Aprili 2018

Yanga yaanza mazoezi Ethiopia


Mabingwa wa Tanzania, Yanga leo wamefanya mazoezi yao ya kwanza nchini Ethiopia. 

Yanga wamefanya mazoezi yao katika mji wa Awassa tayari kujiandaa na mechi yao ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Wolayta Dicha ya nchini humo. 

Mechi hiyo ya pili, itapigwa keshokutwa Jumatano mjini Awassa. 

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi ambaye ameongozana na timu, amesema wamemaliza mazoezi yao salama. 

“Tumemaliza mazoezi salama hapa mjini Awassa na mambo yanakwenda vizuri kabisa,” alisema. 

Katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam, Yanga iliwanyoosha Wahabeshi kwa kuwachapa mabao 2-0. Hivyo inachotakiwa kulinda ushindi wake kwa kupata sare au kushinda tena ili kufuzu katika hatua ya makudi.