HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 7 Mei 2018

Abiria wa Mwendokasi wagoma na Kuandamana Kimara

Leo May 7, 2017 katika kituo cha mabasi ya mwendokasi cha Kimara Mwisho, abiria wa mabasi hayo wamefanya vurugu ikiwa ni pamoja na kuandamana kwenye njia ya mwendokasi.

Shuhuda aliyekuwa eneo hilo Alexander Wencelaus ameeleza kuwa magari yote yaliyokuwa yanapita kituoni hapo yalikuwa yamejaa kiasi cha kutoweza kuchukua abiria wengine kwenye kituo hicho.

Baada ya changamoto hiyo kudumu kwa saa kadhaa ndipo abiria walipoanza kupita kwenye njia ya mwendokasi kwa ‘kuandamana’ wakishinikiza magari yaongezwe ili kutatua changamoto hiyo.

Hata hivyo baada ya muda changamoto hiyo ilitatuliwa kwa magari ya ‘Express’ kuanza kuchukua abiria kituoni hapo na hatimaye shughuli nyingine katika eneo hilo kuendelea kama kawaida.