HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Alhamisi, 3 Mei 2018

Baraka da Prince afunguka kuhusu kujiunga na WCB

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Baraka de Prince amefunguka kuhusu tetesi ambazo zimekuwa zikisambaa kwa muda mrefu sasa kuwa amejiunga na lebo ya WCB.

Tetesi za Baraka kusainiwa WCB zilianza kushika kasi siku za hivi karibuni baada ya kuonekana ana ukaribu na wasanii wa label hiyo na hata wadau wa WCB.

Lakini tetesi hizi zipamba moto zaidi pale Baraka alipodaiwa kutengeneza kiki ya Rommy kumtongoza mpenzi wake Naj kwa lengo la kuitambulisha ngoma yao mpya iliyopewa jina Bora Iwe.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Rick media, Baraka amekana tetesi za yeye kujiunga WCB na kudai ni marafiki tu wa karibu.

Hapana, WCB ni kama familia yangu, mara nyingi hata mameneja wa WCB ndio wanakuwa wananiongoza na kunielekeza nifanye nini. Kwa hiyo tumeamua kuwa kama familia na kuna wasanii wengi wanafanya vizuri, lakini sio kwamba nipo chini ya WCB, no siyo kweli,”alisema Baraka alipoulizwa kama ana mpango wowote wa kujiunga na WCB.

Hapo nyuma Baraka hakuwa na ukaribu na WCB mpaka pale alipojitoa kwenye label ya Rockstar 4000 aliyoko msanii Ali Kiba.