HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatano, 2 Mei 2018

Bill nass na Nand waibuka kivingine

Msanii Bill Nas ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Tagi ubavu' amefunguka na kusema kuwa kuna kazi ambayo amefanya na msanii Nandy na kudai kuwa anaamini wimbo huo utatoka wakati ukifika.

Bill Nas ameweka wazi hayo leo Mei 2, 2018 akiwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa EATV na kudai kuwa yeye na Nandy sasa wanaendelea kuishi kama marafiki na kuwa upo wimbo wamefanya pamoja.

"Kuna wimbo tumefanya pamoja, wimbo umefanywa chini ya S2KIZZY hivyo naamini muda ukifika utatoka tu ila nachojua ni wimbo mkali, kuhusu jambo ambalo limetokea kuhusu mimi na yeye tayari nilishaomba radhi kwa wananchi na sasa maisha ya kawaida yanaendelea, hivyo hatuna tofauti yoyote ile kwa kuwa yule ni rafiki yangu na nina iheshimu sana familia yake akiwa pamoja na mama yake kwa kuwa ni mtu ambaye amekuwa akijitoa sana ku-support kazi za mwanaye" alisema Bill Nas 

Mbali na hilo Bill Nas amedai kuwa katika wasanii wa kike wawili ambao wanafanya vizuri nasi Vanessa Mdee pamoja na Nandy ndiyo wasanii wanaofanya vyema kwa sasa