HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatano, 2 Mei 2018

Magufuli aweka wazi walichokosea Iringa


Rais Dkt. Magufuli amefunguka na kusema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Iringa walikosea sana kwa kuchagua viongozi wala rushwa na kusema hilo ndilo lilikuwa kosa kubwa ndiyo maana hata yeye wakati wa kampeni alikosa wadhamini kwa sababu wote walinunuliwa.

Magufuli amesema hayo leo Mei 2, 2018 akiwa anaweka jiwe la msingi katika hospitali ya wilaya ya Kilolo na kusema anashukuru sasa viongozi hao wa CCM wameanza kuchukua hatua kwa watu hao jambo ambalo anaamini litarudisha uhai wa chama Iringa. 

"Nawakumbusha wenzangu wana CCM kwamba rushwa ni mbaya sana na rushwa Iringa ilitawala kwa sababu mlichagua viongozi wala rushwa ila nina shukuru mmeanza kuwachukulia hatua ila jamani rushwa ni mbaya, na inatuchelewesha na inawanyima haki wale ambao wanastaili kuongozwa, mimi wadhamini wote walinidhamini kutoka hapa Kilolo ndiyo maana siwezi kuwasahau na nilipoaambiwa na Mhe. Jafo kwamba kuna hospitali imekwama tangu mwaka 2011 kwa zaidi ya miaka mitano haijapaya pesa na imesimama na wanataka kujenga hospitalii ya wilaya kubwa na fedha zinazohitajika ni bilioni 4.2 nikasema pelekeni watu kule hawapendi rushwa ni watu wachapakazi"alisema Rais Magufuli 

Katika uchaguzi uliopita, Mchungaji Peter Msigwa alifanikiwa kutetea kiti chake huku chama chake cha CHADEMA kikipata madiwani 14 kati ya kata 18. Kwa matokeo hayo CHADEMA kiliandika historia ya kuongoza halmashauri ya Manispaa ya Iringa. Japo mpaka sasa madiwani kadhaa kutoka CHADEMA wamejiuzulu nafasi zao na kurudi CCM kwa kile wanachodai kuunga mkono juhudu za serikali ya awamu ya tano na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.