Golikipa mkongwe wa Juventus Gianluigi Buffon ametangaza kuondoka kwenye timu hiyo baada ya kuitumikia kwa kipindi cha miaka 17.
Buffon, 40, anatarajia kucheza mchezo wake wa mwisho Jumamosi hii akiwa amevalia jezi ya Juventus, ambao utakuwa wa ligi kuu ya Italia (Serie A) dhidi ya Verona.
Mchezaji huyo ametangaza hilo Alhamisi hii kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ikiwa ni siku nne zimepita tangu alipoiongoza Juve kutwaa kombe la Coppa Italia.
“Jumamosi itakuwa mechi yangu ya mwisho kwa Juventus na kumaliza safari hii na vikombe viwili na pamoja na rais na ulimwengu wote wa Bianconeri kwa upande wangu, utakuwa maalum sana,” amesema Buffon kwenye mkutano huo.
Buffon ameshinda mataji tisa ya Serie A tangu alipoanza kuichezea Juventus mwaka 2001 lakini hajawahi kushinda taji la klabu bingwa Ulaya (UEFA) lakini amewahi kufika fainali mara tatu.