Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeigomea Yanga kuvaa jezi zenye nembo yoyote ya mdhamini leo itakapokabiliana na USM Alger.
Taarifa za kuzuiwa kutumia jezi hizo zimetolewa jana usiku baada ya kukaa kikao cha maandalizi ya mchezo kilichoshirikisha Yanga, USM Alger, waamuzi pamoja na Kamishna wa mchezo huo.
Meneja wa Yanga, Hafidh Salehe alisema kwamba CAF wanahitaji kila klabu iwasilishe taarifa za wadhamini ambao watakuwepo kwenye jezi ya timu husika katika hatua hiyo ya makundi.
"Tulishawatumia taarifa CAF lakini kwa bahati mbaya bado hawajaturudishia majibu hivyo kamisaa ametuambia kwa mechi hii tunatakiwa kutumia jezi ambazo hazina nembo yoyote ya mdhamini hadi CAF watakapoturuhusu," alisema Salehe