Mbonde aliumia goti la kulia katika mechi ya duru la kwanza dhidi ya timu yake ya zamani Mtibwa Sugar, hivyo kuwa nje mpaka sasa.
BEKI wa Simba, Salim Mbonde, amefichua kuwa hawezi kucheza tena mechi yoyote msimu huu kutokana na kusumbuliwa na majeraha badala yake anajipanga upya kwa msimu ujao.
PATA HABARI KWA HARAKA ZAIDI
Download Katisha blog app kwenye simu yako, bonyeza 👇👇👇
Mbonde aliumia goti la kulia katika mechi ya duru la kwanza dhidi ya timu yake ya zamani Mtibwa Sugar, hivyo kuwa nje mpaka sasa.
“Sijawa fiti na ikitokea nikacheza basi itakuwa ni dharura kubwa isiyoepukika, kwani nilipocheza na Njombe Mji ni kama nilijitonesha na kujikuta maumivu yakirejea upya,” alisema.
Licha ya kutokucheza mechi nyingi ndani ya msimu huu, Mbonde amesema hakuna kitu anachokisubiri kwa hamu kama kuvaa medali ya ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.
“Najisikia furaha kucheza Simba kwa msimu wa kwanza tu inapata mafanikio, tuna nafasi ya kutwaa ubingwa uliokosekana kwa miaka mitano, hii ni kumbukumbu za rekodi zangu za maisha ya soka,” alisema.
PATA HABARI KWA HARAKA ZAIDI
Download Katisha blog app kwenye simu yako, bonyeza 👇👇👇