Mchezo huo ni karata ya kwanza ya Yanga kwenye Kundi D la mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambalo, pia zipo timu za Gor Mahia ya Kenya na wawakilishi wa Rwanda, Rayon Sports.
BEKI Andrew Vincent ‘Dante’ na winga Emmanuel Martin wametamba kwamba, hakuna mbinu nje ya uwanja itakayofanywa na wenyeji wao USM Alger inayoweza kuwakatisha tamaa na kuwafanya kupoteza mchezo huo.
PATA HABARI KWA HARAKA ZAIDI Download katisha blog App👇👇Bonyeza hapa👇👇
Download katisha blog App👇👇Bonyeza hapa👇👇
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.katisha.blog
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.katisha.blog
Mchezo huo ni karata ya kwanza ya Yanga kwenye Kundi D la mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambalo, pia zipo timu za Gor Mahia ya Kenya na wawakilishi wa Rwanda, Rayon Sports.
Dante na Martin wameliambia Mwanaspoti, timu kutoka mataifa yanayozungumza Lugha ya Kiarabu na Kifaransa zimekuwa na mbinu chafu za kuwatoa mchezoni wachezaji wa timu pinzani hasa vitisho vya mashabiki, lakini hilo haliwezi kuwatisha kwani wana uzoefu na mechi za kimataifa.
“Tumeshacheza idadi kubwa ya mechi zenye ushindani na presha kubwa kuliko hii, hivyo hao mashabiki hata wafanye nini, sidhani kama tunaweza kutoka mchezoni na kucheza chini ya kiwango,” alisema Martin.
Naye Dante alisema kikubwa ambacho watahakikisha wanakifanya ni mawazo kuelekeza ndani ya eneo la kuchezea tu na sio vinginevyo.
“Kwa suala la mashabiki wenye fujo hilo kwa Waarabu haliepukiki na kama ukiruhusu tu akili yako iwaze mashabiki au nini kinafanyika nje ya uwanja, basi unajiweka matatizoni. Nadhani kikubwa ni kutosikiliza kelele zao na badala yake tuwekeze akili na nguvu uwanjani,” alisema Dante.
Yanga imeshacheza na timu kadhaa za Kiarabu ndani ya misimu mitatu iliyopita baada ya kuchezaji dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria, Atoile du Sahel ya Tunisia na Al Ahly ya Misri.